Friday, February 18, 2011

Yaliyomkuta mlokole porini

Mlokole mmoja alikuwa anafukuzwa na simba porini. Alipojua kuwa hataweza kumwacha simba akamwomba Mungu ili simba yule naye aokoke. Aliamini simba mlokole hatoweza kumla.

"Baba naomba simba huyu aokoke!"

Basi akadondoka chini akasikilizia. Kwa kuwa alikuwa na imani simba yule akaokoka kweli. Akamtia kucha za mgongo na kusali.

"Baba, nakushukuru kwa mlo huu wa mchana........."

No comments:

Post a Comment